Saturday, December 1, 2012

MANCHESTER UNITED YAMWINDA MESUT OZIL

Mesut Ozil katika moja ya mechi za timu yake ya Real Madrid

MANCHESTER, Uingereza
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson atupia jicho lake kwa kiungo wa Real Madrid Mesut Ozil, 24. Mchezaji huyo raia wa Ujerumani amekuwa sio chaguo la kwanza la meneja wa Real Madrid Mreno Jose Maurinho tokea kuwasili kwa Luka Modric toka Tottenham Hotspurs ya Uingereza.

Mesut Ozil akiichezea ujerumani
katikaMashindano ya UEFA
Sir Alex Ferguson anamtaka Ozil kwa udi na uvumba aje kuchukua nafasi ya kiungo mkongwe wa timu hiyo Paul schools, 38. Kwa sasa Scholes anaonekana dhahiri kuchoka na huenda akatangaza kustaafu soka kwa mara ya pili mwishoni mwa msimu huu.

Kwa upande wa Ozil ameonekana hana furaha kwa kutokuwa chaguo la kwanza kwenye klabu yake. Mesut Ozil alijiunga na Real Madrid miaka miwili iliyopita akitokea timu ya Werder Bremen ya Ujerumani kwa ada ya pauni 12 milioni na amekuwa akipokea mshahara wa pauni 110,000 kwa wiki ambazo kwa timu kama Manchester United ni mshahara wa kawaida. Wataalam na wachambuzi wa soka wanatabiri kama Real Madrid itaamua kumuuza Ozil itamuuza kwa ada isiyopungua pauni 24 milioni.

No comments:

Post a Comment