Tuesday, December 2, 2014

WENGER AWAPONDA WANAOTAKA AACHIE NGAZI

Mashabiki wa Arsenal waliochoshwa na matokeo ya klabu yao

London,
Kocha wa timu ya Arsenal mfaransa Arsene Wenger amepinga vikali na kuwabeza wale wanaosema uwezo wake kuongoza kikosi cha timu ya Arsenal umeshuka. Akiongea juu ya bango la tambala lililokuwa likipitishwa na mashabiki wa timu hiyo katika mchezo kati ya timu hiyo na West Bromwich Albion jumamosi iliyopita. Bongo hilo liliandikwa Arsene tunakushukuru kwa kututengenezea kumbukumbu nzuri, lakini umefika wakati wa kutuaga /ujiuzuru (ARSENE THANKS FOR THE MEMORIES BUT IT’S TIME TO SAY GOODBYE).

Arsene Wenger
Kama lilivyosema bango hilo, Wenger alitumia rekodi yake ya mafanikio kuwaponda wale wanaomtaka ajiuzulu. Wanger alisema ameiingiza kwenye 16 bora za Uefa Champions League kwa miaka 15 mfululizo, rekodi ambayo hakuna Klabu iliyoweza kuifikia. Wenger aliendelea kuwaponda wale wanaomwona hana uwezo wa kufundisha klabu kubwa, kwamba amekuwa mwalimu wa klabu mbalimbali kubwa Barani Ulaya tangu mwaka 1983, na kama kuna mtu anadhani hana uwezo basi yeye (Wenger) ni genius kwa kuweza kuficha mapungufu hayo yasionekane kwa muda wote huo.

Shutuma kwa Arsene Wenger zinakuja kutokana na klabu hiyo kutopata vikombe kwa siku za karibuni.  Kwa sasa Arsenal inashika nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment