Friday, November 14, 2014

GARI BOVU LA SIMBA LASHIKA KASI MTEREMKONI

Kocha wa Simba Patrick Phiri
Kocha mkuu wa Simba Sports Club, Mzambia Patrick Phiri amewashukuru mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kwa kuipa sapoti klabu kuwatia nguvu wachezaji kulikowapa hamasa ya kupata ushindi wa kwanza katika msimu huu wa VPL. Akiongea kwa furaha; Phiri amejinasibu kwamba huu ni mwisho wa matokeo ya sare kwa klabu hiyo ambayo imekuwa ikiyapata katika mechi sita za kwanza mfululizo tangu kuanzakwa msimu huu wa VPL.
"Nawashukuru  sana viongozi, wachezaji, pamoja na mashabiki wetu ambao wametupa sapoti hadi kufanikiwa kupata ushindi. Haikuwa rahisi na kwa sasa nasema rasmi kuwa matokeo ya sare baibai kinachofuata ni ushindi kwa kila mechi"
Hadi sasa Simba ina pointi tisa ikiwa nyuma kwa pointi tisa toka kwa vinara wa ligi hiyo ambapo Mzambia huyo bado anaamini timu hiyo itafanya vizuri na hata kuchukua ubingwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment