![]() |
| Justin would you marry me? |
Justin Bieber amevunja rekodi ya Make-A-Wish Foundation pale alipokaa na shabiki wake mwenye umri wa miaka minane (8). Bieber alitumia muda wake na shabiki wake Annalysha Brown - Rafanan na kukubali ombi la uchumba la mtoto huyo ambaye alimuomba Justin amuoe hili ikiwa ni mara ya 200 Bieber kutangaza nia.
![]() |
| You may now kiss the bride!! |
Annalysha anasumbuliwa na ugonjwa wa ini ambao kwa sasa unatishia uhai wake. Kabla ya kukutana na Bieber, Annalysha alitumiwa salamu za krismasi mwezi Desemba 2012 kwamba angeweza kukutana na Bieber katika shoo ya mwanamuziki huyo nguli wa muziki wa pop huko Atlanta Agosti 10, 2013. Baada ya kusubiri hatimae ndoto ya binti huyo ikawa ni kweli pale alipopata nafasi ya kuonana na mtu ampendaye sana ambaye kila akimsikia hupata nafuu ya ugonjwa wake. Mama wa mtoto huyo alimshukuru Justin Bieber kwa kumpunguzia maumivu mtoto wake.


No comments:
Post a Comment