![]() |
| Raz-B baada ya kushambuliwa na chupa. |
Mwanamuziki wa zamani wa kundi la B2K, Raz-B amelazwa hospitali nchini China baada ya kupigwa chupa na mlinzi wake (mshikaji). Hali yake imebadilika leo na amepoteza fahamu. Raz-B(28) alikuwa akipiga shoo katika klabu ya usiku na ghafla kulitokea mapigano upande wa mashabiki wakipigana ngumi, na alipojaribu kutuliza hali ghafla alikumbana na maswaibu hayo.
Chupa aliyopigwa nayo ilimtoboa tundu refu kwenye mdomo na alisikika akilalamikia maumivu makali. Raz-B pia alishukuru kwa kuwahishwa hospitali. Alisema:
"F**k this s**t hurts. I have a f**king hole in my lip. Thank God I made it to the hospital"
![]() |
| Raz-B |
Jana, aliruhusiwa baada ya kushonwa nyuzi kazaa mdomoni, lakini alishindwa kuamka asubuhi ya leo ambapo wacheza shoo wake walimuwahisha hospitali haraka. Raz-B aliwahi ku-hit akiwa na kundi la B2K kipindi hicho akiwa na Omarion, Lil' Fizz, na J-Boog wakiwa na ngoma zao kali kama "Bump Bump Bump", "Why I love you", na "Girlfriend".
Chanzo: TMZ


No comments:
Post a Comment