Klabu ya ligi kuu ya Uingereza, Liverpool imemnasa beki wa kushoto wa Valencia Aly Cissokho (25) kwa mkopo wa msimu mmoja.

Mfaransa huyo anatazamiwa kutoa ushindani kwa Jose Enrique ambaye alisajiriwa msimu uliopita akitokea klabu ya NewCastle United ambaye kwa sasa ndiye anamiliki shavu la kushoto la timu hiyo. Cissoko ataenda Merseyside wiki ijayo kwa ajili ya vipimo na majadiliano ya maslahi binafsi.

No comments:
Post a Comment