![]() |
| Mashabiki wa Arsenal waliochoshwa na matokeo ya klabu yao |
London,
Kocha wa timu ya Arsenal
mfaransa Arsene Wenger amepinga vikali na kuwabeza wale wanaosema uwezo wake
kuongoza kikosi cha timu ya Arsenal umeshuka. Akiongea juu ya bango la tambala
lililokuwa likipitishwa na mashabiki wa timu hiyo katika mchezo kati ya timu
hiyo na West Bromwich Albion jumamosi iliyopita. Bongo hilo liliandikwa Arsene
tunakushukuru kwa kututengenezea kumbukumbu nzuri, lakini umefika wakati wa
kutuaga /ujiuzuru (ARSENE THANKS FOR THE MEMORIES BUT IT’S TIME TO SAY GOODBYE).
![]() |
| Arsene Wenger |
Kama lilivyosema bango hilo,
Wenger alitumia rekodi yake ya mafanikio kuwaponda wale wanaomtaka ajiuzulu. Wanger
alisema ameiingiza kwenye 16 bora za Uefa Champions
League kwa miaka 15 mfululizo, rekodi ambayo hakuna Klabu iliyoweza kuifikia. Wenger
aliendelea kuwaponda wale wanaomwona hana uwezo wa kufundisha klabu kubwa,
kwamba amekuwa mwalimu wa klabu mbalimbali kubwa Barani Ulaya tangu mwaka 1983,
na kama kuna mtu anadhani hana uwezo basi yeye (Wenger) ni genius kwa kuweza
kuficha mapungufu hayo yasionekane kwa muda wote huo.









