![]() |
| Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Paulsen |
Harambee Stars ya Kenya jana
iliwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza tayari kwa mchezo wake wa leo dhidi
ya Taifa Stars. Kocha mkuu wa Wakenya hao Henri Michel amejinadi kuwa atatumia
kikosi kilekile kilichoisumbua Afrika Kusini katika mchezo wa kirafiki
uliochezwa Oktoba 16 katika uwanja wa Nyayo. Katika mchezo huo Afrika Kusini
ilipata ushindi mwembamba wa mabao 2-1.
Harambee Stars imewasili bila ya
kipa wake namba moja Arnold Origi aneyekipiga katika timu ya Ullkisa amabaye
amebanwa na ratiba ngumu ya ligi. Pia Wakenya hao watamkosa mshambuliaji wao
hatari Victor Wanyama ambaye anakabiliwa na majeruhi. Michel amemuita Jactone
Odhiambo wa Ulinzi kuziba pengo la Origin a Anthony Akumu wa Gor Mahia kuziba
pengo la Wanyama.
Naye kocha wa Taifa Stars Kim
Paulsen amefanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi chake kwa kuwaacha Said
Bahanuzi (Yanga) na Haruna Moshi “Boban” (Simba). Paulsen ameongeza kiungo
hatari Amri Kiemba (Simba) pamoja na damu changa kama Frank Domayo (Yanga),
Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba). Pia katika kikosi hicho
hakuwaacha wachezaji wenye asili ya visiwani ambao wataruhusiwa kujiunga na
Zanzibar Heroes mara tu baada ya mchezo wa Leo. Wachezaji hao ni Aggrey Morris,
Said Nassor “Cholo”, na Issa Rashid.

No comments:
Post a Comment