![]() |
| Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Picha kwa hisani ya tff.or,tz |
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars inatazamia kushuka katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza kesho jumatano tarehe 14 itakapo wakaribisha Harambee Stars ya Kenya. Taifa Stars na Harambee Stars zitakwaana katika mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Kwa mujibu wa mtandao wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Tanzania tff.or.tz, mchezo huo unatazamiwa kuanza majira ya saa 10 jioni. Mchezo huu ni muhimu kwa timu zote mbili, ambapo kwa upande wa Kenya itakuwa ikijipima nguvu kujiandaa na mchezo wa hatua ya makundi wa kuwania nafasi ya kushiriki kombe la dunia na pia kama ilivyo kwa Taifa Stars pia mchezo huo ni maandalizi ya michuano ya kombe la CECAFA Challenge.
Taifa Stars kwa sasa ipo katika nafasi ya 134 katika viwango vya soka duniani, itaingia dimbani kuchuana na Kenya iliyo katika nafasi ya 130. Mbali na maandalizi ya CECAFA Challenge Cup, mchezo huo ni muhimu kwa Stars inayopigana kurejea katika kiwango chake juu, ambapo katika historia ni nafasi ya 65 ambayo ilifikiwa mnamo mwaka 1965.

No comments:
Post a Comment