![]() |
| Roberto Di Matteo akifuatilia moja ya michezo alipokuwa kocha wa Chelsea |
Chelsea
imetangaza kumtema maeneja wake Mtaliano Roberto Di Matteo kwa kilichoelezwa
kutokuonesha mwenendo mzuri wa timu. Di Matteo mabaye katika uongozi wake
klabuni hapo aliingoza Chelsea maarufu kama “The Blues”michezo 42 ambapo
ilishinda 24, kupoteza 9 na kutoka sare 9. Kufutwa kazi kwa Di Matteo's kulitazamiwa
kufuatia klabu hiyo ya London kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Juventus na
kuifanya kuwa bingwa mtetezi wa kwanza kutolewa katika hatua ya makundi katika
historia ya mashindano ya klabu bingwa barani ulaya (UEFA Champions League).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotelewa na mtandao wa klabu
www.chelseafc.com,
klabu hiyo yenye uwanja wake Stanford Bridge imethibitisha kuondoka kwa Di Matteo.
Sehemu ya taarifa ilisema Chelsea imevunja mkataba na na meneja Roberto Di
Matteo. Kiwango cha mchezo na matokeo ya timu kwa siku za karibuni yamekuwa
hayaridhishi na mmiliki na bodi wameona mabadiliko ni lazima yafanyike sasa
kuiwezesha klabu kuelekea kwenye mwelekeo sahihi kwa kuwa ikielekea kwenye
kipindi muhimu zaidi cha msimu.
![]() |
| Roberto Di Matteo akisherehekea ubingwa wa UEFA Champions League na wapenzi wa Chelsea jijini London |
Klabu
hiyo ilikumbana na wakati mgumu wakati ikitafuta nafasi ya kuingia katika hatua
ya makundi za ligi ya mabingwa huku ikiendelea kupigana kubakia katika nafasi
za juu katika ligi ya nyumbani. Lengo la klabu ni kubakia katika nafasi ya
kiushandani zaidi katika mashindano yote ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
![]() |
| Roberto Di Matteo alipokuwa mchezaji wa Chelsea |
Pia
klabu hiyo imemshukuru meneja huyokwa yote mazuri aliyoifanyia klabu hiyo kubwa
hasa likiwa ni kuiwezesha kuchukua ubingwa katika ligi ya klabu bingwa barani
ulaya sanjari na kuipa ushindi wa kombe la chama cha soka cha Uingereza (FA
Cup). Klabu hiyo inasema haitaweza kumsahau Muitaliano huyo kwa mchango wake
mkubwa alioutoa ambao ni wa kihistoria katika klabu hiyo na imesema iko tayari
kumkaribisha muda wowote ule.
Wakati
huohuo klabu hiyo ikitazamiwa kumtangaza
kocha mpya wa klabu hiyo baada ya kumfukuza kazi Di Matteo, kumekuwa na kundi
linalomlaumu Di Matteo kwa matokeo mabaya katika michezo ya hivi karibuni. Katika
michezo nane ya mwisho aliwaongoza wazee wa ‘darajani’ kushinda michezo ,miwili
tu kitu kilichomplekea mmiliki wa klabu hiyo asiye mvumilivu Roman Abramovich kumfukuza
kazi.



No comments:
Post a Comment