Wednesday, November 14, 2012

LEON OSMAN: SIJAKATA TAMAA KUCHEZEA ENGLAND

Leon Osman

Kiungo wa Everton anayemalizia mpira wake na kuonekana kuelekea ukingoni mwa kipaji chake Leon Osman (31) amesema hajakata tamaa na hatakata tamaa. Osman anategemea kucheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa baada ya kuitwa kwa mara ya kwanza na kocha wa Uingereza Roy Hogson.

Leon Osman katika moja ya mechi za watani wa jadi (Derby Match) dhidi ya 
Liverpool
England baadae leo itapambana na Sweden katika mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na FIFA utakaofanyika jijini Stockholm, Sweden. Leon Osman amejumuishwa kwenye kikosi cha England kilichoenda Stockholm.

No comments:

Post a Comment