![]() |
| Timu ya taifa ya Kenya "Harambee Stars" |
Timu ya soka ya Uganda The Cranes
itashuka dimbani kuikaribisha timu ya taifa ya Kenya almaarufu Harambee Stars.
Timu hizi zitachuana katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya CECAFA Challenge
Cup mchezo utakaochezwa tarehe 24 Novemba mwaka huu jijini Kampala.
![]() |
| Timu ya taifa ya Uganda "The Cranes" |
The cranes bado wana uchungu wa
kubaniwa na Harambee Stars nafasi ya kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika. Katika
mchezo huo Wakenya hao waliilazimisha The Cranes sare isiyo na magoli (suluhu),
mchezo huo ulifanyika huko Namboole. The Cranes pia katika mchezo wake wa
mwisho ilifungwa kwa penati 8-9 na Zambia hapohapo Namboole mwezi Januari mwaka
huu.
Kabla ya mechi hiyo ya ufunguzi
timu za Ethiopia na Sudani Kusini zitapambana katika mchezo unaotazamiwa kuanza
majiara ya saa tisa (9) alasiri kwa saa za Afrika Mashariki. Kwa sasa Uganda
ipo katika nafasi ya 88 na Kenya ipo katika nafasi ya 130 ya ubora wa viwango
vya soka duniani.


No comments:
Post a Comment