Monday, November 19, 2012

HAYATOU KUTUA UGANDA

Rais wa CAF: Issa Hayatou
Rais wa shirikisho la soka la barani Africa (CUF) Issa Hayatou aukubali mwaliko wa shirikisho la soka la Uganda (FUFA) na CECAFA kwenda nchini Uganda. Kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho la soka la Uganda Hayatou anategemewa kuwasili nchini humo tarehe 22 Novemba (Alhamisi) majira ya jioni kufuatia mwaliko maalum aliopokea toka kwa rais wa shirikisho la soka la Uganda Lawrence Mulindwa na rais wa CECAFA Eng. Leodgar Tenga.

Rais wa Shirikisho la Soka la Jamhuri ya
 Kidemokrasia ya Congo nduguCostant Omari Seleman
Katibu Mkuu wa CAF Hicham El Amrani
Makamu wa Rais CAF: Mohamed Raouraoua 
Katika ziara hiyo Hayatou atafuatana na maofisa mbalimbali wa CAF. Miongoni mwa atakaombatana nao ni Katibu Mkuu wa CAF Hicham El Amran wengine waliothibitisha ni Mohamed Raouraoua, Costant Omari na Ngangue Appolinaire. Mara tu baada ya kuwasili na msafara wake anatazamiwa kukutana na Watendaji wa FUFA jijini  Kampala. Ijumaa tarehe 23 Novemba, atahudhuria CECAFA Congress katika hoteli ya Serena. Hayatou anatazamiwa kuwa kusimamia ufunguzi rasmi wa CECAFA Tusker Cup  katika uwanja wa Namboole siku ya jumamosi tarehe 24, Novemba. Hayatou pia anatazamiwa kukutana na waziri wa michezo wa Uganda Mheshimiwa Charles Bukalindi kwa mazungumzo mafupi.

No comments:

Post a Comment