![]() |
| Sir Richard 'Ricky' Hatton |
Bondia Mwingereza Ricky Hatton (34) ametangaza kustaafu tena kwa
mara ya pili baada ya jaribio lake la kurudi tena kwenye masumbwi kushindwa.
Katika pambano lake la kurudi kwenye mchezo huu aliambulia kichapo kikali
alipopigwa kwa ‘knockout’ na Vyacheslav Senchenko wa Ukraini jijini Manchester
Uingereza jumamosi iliyopita.
Mashabiki wapatao 20,000 walijitokeza kuja kushuhudia kurudi kwa
bingwa huyo wa zamani wa dunia katika mji wake wa nyumbani. Ricky alianza
pambano hilo vizuri lakini alionekana kuchoka kadri muda ulivyokuwa ukisonga
mbele na kumpa nafasi Senchenko (35) kumtupia makonde makali. Ricky alilamba
mchanga na alipohesabiwa alishindwa kuinuka na kumfanya mwamuzi kumpa ushindi
Senchenko. Senchenko ameendelea kuboresha rekodi yake ambapo hadi sasa amepoteza
pambano moja (1)tu kati ya thelasini na nne (34) aliyocheza.
![]() |
| Sir Richard Hatton akionesha moja ya mikanda yake |
![]() |
| Sir Richard 'Ricky' Hatton akiaga mashabiki alipotangaza kustaafu kwa mara ya pili |
Akiongea baada ya pambano Hatton alisema"nilitaka walau
pambano moja zaidi kuona kama naweza kurejea, na nimeona sintoweza, nimeona
sina uwezo tena.” "Nimejiangalia kwenye kioo na nikajiambia mwenyewe
nimejitahidi, na sijilaumu”.



No comments:
Post a Comment