Thursday, November 8, 2012

Messi Asikitikia Nafasi Zilizopotezwa Barca Ikichezea Kichapo cha 2-1


Lionel Messi ameilaumu timu yake pale iliposhtukizwa na kichapo cha mabao 2-1 wakati ilipochuana nan timu ya Celtic ya Uskochi katika mpambano wa Ligi ya Mabingwa ya Ulaya maarufa kama UEFA Champions League. Mchezaji huyo nguli wa timu ya Barcelona amelaumu umaliaziaji mbovu pale timu yake ilipokuwa ikilisogelea lango la wapinzani wao na kupelekea vigogo hao wa soka wa Hispania na kupoteza mchezo wa hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika miaka kipindi cha mika mitatu.

Messi anakiri kuwa pamoja na Barcelona's kuonesha kiwango bora cha mchezo wa jana ikiwa ugenini kulinganisha na mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana katika dimba la Camp Nou (nyumbani Barcelona) ilipopata ushindi wa mabao mawili kwa moja; bado vinara hao wa ligi ya kuu ya soka ya Hispania walipoteza nafasi nyingi kupitia kwa Messi mwenyewe, Sanchez, Xavi, naIniesta. Katika mchezo huo washambualiaji Lionel Messi na Alexis Sanchez kila mmoja aligonga mwamba mara moja huku kipa namba tatu wa zamani wa Newcastle United akiokoa michomo mingi iliyokuwa ikielekezwa katika lango la Celtic. Katika mchezo huo Scotland Celtic ilianza kufumania nyavu za wapinzani wao kupitia kwa mshambuliaji wao Mkenya Victor Wanyama na baadae kuongeza bao la pili kupitia kwa Tony Watt kabla ya Lionel Messi kuipatia Barca bao la kufutia machozi huku muda ukiwa umeyoyoma.
Messi amesema Celtic katika michezo yote miwili wameonesha uwezo mzuri kwa kucheza kwa kujihami zaidi na kufanya mashambulizi ya kushitukiza, pia wameonekana kuimarika zaidi katika kucheza mipira ya kona, na pasi ndefu na kwa jinsi hiyo wamekuwa wakipata mabao yao. Naye Kocha wa Barca Tito Villanova kwa upande wake ameipongeza Celtic kwa ushindi huo ingawa ametofautiana mshambuliaji wake kwa kusema kwamba hana la kuwalaumu wachezaji wake kwa yaliyotokea katika mchezo huo. Villanova anakiri kuwa waliusoma mchezo na walikuwa wakijua nini wanafanya na kuwawezesha kutengeneza nafasi nyingi ingiwa hawakumalizia vizuri. Villanova amemsifu kipa wa Celtic kwa kuokoa mipira ya hatari ya wachezaji wake huku akisema ingawa hapendi kufungwa lakini hakukuwa na la ziada na hivyo amyakubalia matokeo hayo.
Kwa matokeo hayo Barcelona bado inaendelea kushilia uongozi wa kundi hilo (kundi G) huku Celtic ikipaa hadi nafasi ya pili juu Benfica na Spartak Moscoc.
Habari na picha kwa mujibu wa ESPN

1 comment: