Thursday, November 22, 2012

MAN CITY YALAMBA MCHANGA

Kocha wa Man City Roberto Mancini

Mabingwa wa Uingereza Manchester City jana waliaga rasmi michuano ya klabu bingwa barani ulaya kwa mara ya pili mfululizo. Bao la mapema la Mfaransa Karima Benzema aliloifungia timu yake ya Real Madrid ya Hispania liliweza kuikatisha ndoto ya Man City kuingia hatua ya 16 bora ya michuano hiyo. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 bao lakusawazisha la Man City likifungwa Sergio Kun Aguero kwa njia ya penati dakika 15 kabla ya mchezo kumalizika baada ya kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari na Alvaro Alberoa ambaye alitolewa kwa kadi nyekundu.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger

Wakati huo huo Arsenal ilikata tiketi yake kwenye hatua ya 16 bora baada ya kuwafunga mabingwa wa Ufaransa Montpellier kwa mabao 2-0. Mabao hayo yalifungwa na Jack wilshere na Lukas Podolski.

No comments:

Post a Comment