MANACOR, Hispania
![]() |
| Rafa Nadal Akijifua |
Mchezaji nguli wa mchezo wa tennis Rafa
Nadal wa Hispania ameanza kufanya mazoezi madogo madogo na kucheza uwanjani.
Rafa ameonesha kupona na kuimarika kwa goti lake ambapo jumanne hii (jana) alianza
mazoezi, hii ikiwa ni mara ya kwanza toka mwezi Agosti mwaka huu alipolazimika
kujitoa kwenye michuano ya U.S. Open.
Nadal (26) amekuwa nje ya uwanja na
hajashiriki mashindano yoyote yale tokea mwezi Juni mwaka huu alipotolewa na
Czech Lukas Rosol katika raundi ya pili ya michuano ya Wimbledon. Rafa ambaye
ni bingwa mara 11 wa gland slam kwa mchezaji mmoja mmoja ameanza mazoezi chini
ya kocha wake ambaye pia ni ndugu wa baba yake Toni Nadal huko nyumbani kwao
Manacor katika kisiwa cha Majorca. Pamoja na kuwa nje ya uwanja kwa kipindi
chote hicho bado yupo katika nafasi ya nne (4) katika msimamamo wa wachezaji
bora wa kiume duniani.
![]() |
| Rafa Nadal akisalimia Mashabiki |
Rafa
Nadal anatazamiwa kurejea kwenye michezo ya mashindano mwezi Januari mwakani
wakati wa michuano ya Australian Open. Akiongea na shirika la habari la
Uingereza (Reuters) alisema
anajisikia vizuri na goti lake limeimarika vizuri na anafuraha kurudi uwanjani
kwa mara nyingine baada ya miezi kadhaa. Anafurahia kujisikia tena nikicheza
tennis kwa mara nyingine na vyema, kitakuwa ni kipindi kingine cha kupona
kwangu, aliongeza.
![]() |
| Rafa Nadal Akiwa na moja ya vikombe vyake |
Ameaza taratibu na anaendelea
kila siku. Atajituma katika mazoezi ili arudi uwanjani na anategemea goti lake
litapona kabisa hivi karibuni. Siku zote anatakiwa kuwa makini. Hasa akiwa amekaa
kwa miezi kadhaa nje ya uwanja mwili unatakiwa uanze kuzoea kila kitu cha ndani
ya uwanja na misuli nayo inatakiwa izoeshwe kwa taratibu zaidi Nadal aliongeza.



No comments:
Post a Comment