Saturday, December 1, 2012
Dumu Sports: MANCHESTER UNITED YAMWINDA MESUT OZIL
Dumu Sports: MANCHESTER UNITED YAMWINDA MESUT OZIL: Mesut Ozil katika moja ya mechi za timu yake ya Real Madrid MANCHESTER , Uingereza Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson atu...
MANCHESTER UNITED YAMWINDA MESUT OZIL
![]() |
| Mesut Ozil katika moja ya mechi za timu yake ya Real Madrid |
MANCHESTER, Uingereza
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson atupia jicho lake kwa
kiungo wa Real Madrid Mesut Ozil, 24. Mchezaji huyo raia wa Ujerumani amekuwa
sio chaguo la kwanza la meneja wa Real Madrid Mreno Jose Maurinho tokea
kuwasili kwa Luka Modric toka Tottenham Hotspurs ya Uingereza.
![]() |
| Mesut Ozil akiichezea ujerumani katikaMashindano ya UEFA |
Sir Alex Ferguson anamtaka Ozil kwa udi na uvumba aje kuchukua nafasi ya
kiungo mkongwe wa timu hiyo Paul schools, 38. Kwa sasa Scholes anaonekana
dhahiri kuchoka na huenda akatangaza kustaafu soka kwa mara ya pili mwishoni
mwa msimu huu.
Kwa upande wa Ozil ameonekana hana furaha kwa kutokuwa chaguo la kwanza
kwenye klabu yake. Mesut Ozil alijiunga na Real Madrid miaka miwili iliyopita
akitokea timu ya Werder Bremen ya Ujerumani kwa ada ya pauni 12 milioni na
amekuwa akipokea mshahara wa pauni 110,000 kwa wiki ambazo kwa timu kama
Manchester United ni mshahara wa kawaida. Wataalam na wachambuzi wa soka
wanatabiri kama Real Madrid itaamua kumuuza Ozil itamuuza kwa ada isiyopungua
pauni 24 milioni.
Dumu Sports: LUIS SUAREZ ASHINDA BARCLAYS GOLDEN BOOT 10 - GOAL...
Dumu Sports: LUIS SUAREZ ASHINDA BARCLAYS GOLDEN BOOT 10 - GOAL...: Uingereza, Mshambuliaji wa timu ya Liverpool Luis Suarez ameshinda Barclays Golden Boot baada ya kuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufik...
LUIS SUAREZ ASHINDA BARCLAYS GOLDEN BOOT 10 - GOAL AWARD
Uingereza,
Mshambuliaji wa timu ya Liverpool Luis Suarez ameshinda Barclays Golden Boot baada ya kuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufikisha mabao kumi. Suarez amefikisha mabao hayo katika michezo 13 aliyoichezea timu yake ya Liverpool msimu huu.
Akiongea baada ya kupokea zawadi hiyo, Suarez alimshukuru meneja wake
Brendan Rodgers kwa kumchochea kuongeza juhudi sio kwake yeye tu bali kwa kila
mchezaji wa timu ya Liverpool. Pia alisema meneja wake anamchezesha kwa staili
anayoipenda kwa kumfanya kuwa mshambuliaji huru na pekee kwenye kikosi sanjari
na kumtia moyo kwamba atafunga mabao kitu ambacho kimemuongezea kujiamini.
Pia aliwapongeza viungo washambuliaji vijana wa timu hiyo Raheem
Sterling na Suso kwa viwango vyao na jinsi wanavyojifunza toka kwa wachezaji
wazoefu kama Steven Gerrard, Pepe Reina na Jamie Carragher na watakuja
kufanikiwa sana siku za baadae.
Friday, November 30, 2012
Dumu Sports: MAVAZI YA MICHAEL JORDAN YACHAFUA HEWA KWENYE GOLF...
Dumu Sports: MAVAZI YA MICHAEL JORDAN YACHAFUA HEWA KWENYE GOLF...: California , Marekani Mavazi ya Michael Jordan yawa kituko kwenye viwanja vya mchezo wa golf. Tangu ajiunge na mchezo huo amekuwa akivaa...
MAVAZI YA MICHAEL JORDAN YACHAFUA HEWA KWENYE GOLF
ADIOS HECTOR "MACHO" CAMACHO
![]() |
| Mama wa marehemu Hector "Macho" Camacho, Maria Matias akilia "wamemuua, wamuuaa" wakati akitoa heshima ya mwisho |
SAN JUAN, Puerto Rico
Mabondia, wapenzi wa
ngumi, na wanandugu wa bondia Hector “Macho” juzi (jumanne) kuuaga na kuuzika
mwili wa mwanamasumbwi nguli. Waombolezaji waliobeba picha mbalimbali za Macho
walipita mbele ya jeneza lake kumuaga marehemu.
![]() |
| waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Hector "Macho" Camacho |
Wakiongozwa na familia ya
marehemu wakiongozwa na mama wa marehemu Maria Matia walitoa heshima za mwisho.
Camacho aliuawa tarehe 20 Novemba akiwa kwenye maegesho ya magari ya bar moja
katika mji wa Bayamon nchini Purto Rico. Katika tukio hilo rafiki yake wa
karibu alifariki papo hapo na Camacho alifariki siku tatu baadaye akiwa kwenye
matibabu.
Hadi sasa polisi nchini
humo wanasema wana orodha ya washukiwa lakini bado hawajawatia mbaroni.
Thursday, November 29, 2012
NOVAK DJOKOVIC NA KUERTEN WAFUNGA KATIKA MECHI YA SOKA BRAZIL
RIO DE JANEIRO, Brazil
![]() |
| Novak Djokovic kulia akishangilia na Bebeto katikati na Edilson wa Brazil |
Nyota wa
mchezo wa tennis Novak Djokovic na bingwa mara tatu wa French Open Gustavo Kuerten walifunga katika mchezo wa kuchangisha fedha ulichezwa
kabla ya mchezo wa ligi ya mpira wa miguu ya Brazil siku ya Jumapili tarehe 18
Novemba mwaka huu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la
Associated Press mchezo huo uliandaliwa na rafiki wa Djokovic , Mserbia
mwenzake, Dejan Petkovic ambaye amekuwa akifuatilia michezo ya timu mbalimbali
za Brazil kwa zaidi ya muongo mmoja. Katika mchezo huo wachezaji wa zamani wa
timu ya taifa ya Brazili Zico na Bebeto walishiriki.
![]() |
| Novak Djokovic akishangilia na Bebeto wa Brazil |
Katika mchezo huo uliofanyika katika
uwanja wa Engenhao ukitangulia mchezo wa Ubingwa wa Ligi ya Mpira wa Miguu ya
Brazili kati ya Fluminense na Cruzeiro, uliishia kwa matokeo ya 3-3.
Dumu Sports: NADAL KUREJEA UWANJANI AUSTRALIAN OPEN
Dumu Sports: NADAL KUREJEA UWANJANI AUSTRALIAN OPEN: MANACOR , Hispania Rafa Nadal Akijifua Mchezaji nguli wa mchezo wa tennis Rafa Nadal wa Hispania ameanza kufanya mazoezi madogo mado...
NADAL KUREJEA UWANJANI AUSTRALIAN OPEN
MANACOR, Hispania
![]() |
| Rafa Nadal Akijifua |
Mchezaji nguli wa mchezo wa tennis Rafa
Nadal wa Hispania ameanza kufanya mazoezi madogo madogo na kucheza uwanjani.
Rafa ameonesha kupona na kuimarika kwa goti lake ambapo jumanne hii (jana) alianza
mazoezi, hii ikiwa ni mara ya kwanza toka mwezi Agosti mwaka huu alipolazimika
kujitoa kwenye michuano ya U.S. Open.
Nadal (26) amekuwa nje ya uwanja na
hajashiriki mashindano yoyote yale tokea mwezi Juni mwaka huu alipotolewa na
Czech Lukas Rosol katika raundi ya pili ya michuano ya Wimbledon. Rafa ambaye
ni bingwa mara 11 wa gland slam kwa mchezaji mmoja mmoja ameanza mazoezi chini
ya kocha wake ambaye pia ni ndugu wa baba yake Toni Nadal huko nyumbani kwao
Manacor katika kisiwa cha Majorca. Pamoja na kuwa nje ya uwanja kwa kipindi
chote hicho bado yupo katika nafasi ya nne (4) katika msimamamo wa wachezaji
bora wa kiume duniani.
![]() |
| Rafa Nadal akisalimia Mashabiki |
Rafa
Nadal anatazamiwa kurejea kwenye michezo ya mashindano mwezi Januari mwakani
wakati wa michuano ya Australian Open. Akiongea na shirika la habari la
Uingereza (Reuters) alisema
anajisikia vizuri na goti lake limeimarika vizuri na anafuraha kurudi uwanjani
kwa mara nyingine baada ya miezi kadhaa. Anafurahia kujisikia tena nikicheza
tennis kwa mara nyingine na vyema, kitakuwa ni kipindi kingine cha kupona
kwangu, aliongeza.
![]() |
| Rafa Nadal Akiwa na moja ya vikombe vyake |
Ameaza taratibu na anaendelea
kila siku. Atajituma katika mazoezi ili arudi uwanjani na anategemea goti lake
litapona kabisa hivi karibuni. Siku zote anatakiwa kuwa makini. Hasa akiwa amekaa
kwa miezi kadhaa nje ya uwanja mwili unatakiwa uanze kuzoea kila kitu cha ndani
ya uwanja na misuli nayo inatakiwa izoeshwe kwa taratibu zaidi Nadal aliongeza.
Tuesday, November 27, 2012
Dumu Sports: RICKY HATTON ASTAAFU BAADA YA KUPIGWA TENA
Dumu Sports: RICKY HATTON ASTAAFU BAADA YA KUPIGWA TENA: Manchester Sir Richard 'Ricky' Hatton Bondia Mwingereza Ricky Hatton (34) ametangaza kustaafu tena kwa mara ya pili baada ya jaribio ...
RICKY HATTON ASTAAFU BAADA YA KUPIGWA TENA
Manchester
![]() |
| Sir Richard 'Ricky' Hatton |
Bondia Mwingereza Ricky Hatton (34) ametangaza kustaafu tena kwa
mara ya pili baada ya jaribio lake la kurudi tena kwenye masumbwi kushindwa.
Katika pambano lake la kurudi kwenye mchezo huu aliambulia kichapo kikali
alipopigwa kwa ‘knockout’ na Vyacheslav Senchenko wa Ukraini jijini Manchester
Uingereza jumamosi iliyopita.
Mashabiki wapatao 20,000 walijitokeza kuja kushuhudia kurudi kwa
bingwa huyo wa zamani wa dunia katika mji wake wa nyumbani. Ricky alianza
pambano hilo vizuri lakini alionekana kuchoka kadri muda ulivyokuwa ukisonga
mbele na kumpa nafasi Senchenko (35) kumtupia makonde makali. Ricky alilamba
mchanga na alipohesabiwa alishindwa kuinuka na kumfanya mwamuzi kumpa ushindi
Senchenko. Senchenko ameendelea kuboresha rekodi yake ambapo hadi sasa amepoteza
pambano moja (1)tu kati ya thelasini na nne (34) aliyocheza.
![]() |
| Sir Richard Hatton akionesha moja ya mikanda yake |
![]() |
| Sir Richard 'Ricky' Hatton akiaga mashabiki alipotangaza kustaafu kwa mara ya pili |
Akiongea baada ya pambano Hatton alisema"nilitaka walau
pambano moja zaidi kuona kama naweza kurejea, na nimeona sintoweza, nimeona
sina uwezo tena.” "Nimejiangalia kwenye kioo na nikajiambia mwenyewe
nimejitahidi, na sijilaumu”.
Monday, November 26, 2012
Dumu Sports: REKODI BORA KWA MABONDIA CHINI YA MIAKA 25
Dumu Sports: REKODI BORA KWA MABONDIA CHINI YA MIAKA 25: 1. Adrien Broner (25-0, 21 KOs), Age: 23 2. Saul Alvarez (41-0-1, 30 KOs), Age: 22 3. Danny Garcia (25-0, 16 KOs), Age: 24 ...
'MACHO' CAMACHO AFARIKI DUNIA
SAN JUAN, Puerto Rico
![]() |
| Hector 'Macho' Camacho katikati akiwa na warembo |
![]() |
| Amy Camacho mke wa Hector 'Macho' Camacho |
Hector
''Macho'' Camacho katika uhai wake alikuwa ni bondia anayejituma na kujiamini mwenye
ngumi nzito na mtindo wa kujituma katika mapambano yake na mtukutu nje ya
uwanja. Hector ‘Macho’ Camacho alikutwa amefariki siku ya jumamosi baada ya
kuvamiwa katika sehemu ya kuegeshea magari katika mji wa Bayamon huko Puerto
Rico ambako ndiko alikozaliwa. Polisi walikuta pakti za madawa ya kulevya aina
ya cocaine katika gari alilokuwemo.
Camacho, amefariki akiwa na umri wa miaka 50, atakumbukwa kwa
uwezo wake mkubwa wa kuburudisha na kupendwa na mashabiki ambapo walikuwa
wakimpokea kwa kibwagizo ''It's Macho time!'' kabla hajapanda ulingoni. Camacho
alikuwa na kipaji na mbinu zilizowatisha na wapinzani wake na kumfanya kuwa
bondia wa kiwango cha juu katika kipindi hicho.
![]() |
| Enzi za ujana wake |
![]() |
| Macho akipelekwa hospitali |
Macho alipigana kwa kipindi cha miongo mitatu tokaea pambano
lake la kwanza dhidi ya David Brown jijini New York mwaka 1980 hadi pambano
lake dhidi ya Saul Duran huko Kissimmee, Florida, mwaka 2010. Katika uhai wake
alipambana na mabondia nyota mbalimbali wakiwamo Sugar Ray Leonard, Felix
Trinidad, Oscar De La Hoya, Roberto Duran na wengineo wengi.
HII NI KITU NYINGINE
Acky: Msanii wa filamu nchini Tanzania John Stephano Mag...
Acky: Msanii wa filamu nchini Tanzania John Stephano Mag...: HABARI: Msanii wa filamu nchini Tanzania John Stephano Maganga afariki dunia katika hospital ya Muhimbili kutokana na Ugonjwa wa ...
REKODI BORA KWA MABONDIA CHINI YA MIAKA 25
1. Adrien Broner (25-0, 21 KOs), Age: 23
2. Saul Alvarez (41-0-1, 30 KOs), Age: 22
3. Danny Garcia (25-0, 16 KOs), Age: 24
4. Tyson Fury (19-0, 14 KOs), Age: 24
5. Leo Santa Cruz (22-0-1, 13 KOs), Age: 24
6. Miguel Angel Garcia (30-0, 26 KOs), Age: 24
7. George Groves (15-0, 12 KOs), Age: 24
8. Javier Fortuna (20-0, 15 KOs), Age: 23
9. Kazuto Ioka (10-0, 6 KOs), Age: 23
10.
Thomas Oosthuizen (21-0-1, 13 KOs), Age: 24
Sunday, November 25, 2012
Saturday, November 24, 2012
Thursday, November 22, 2012
BEN ARFA, MESSI, NEYMAR, NA FALCAO KUCHUANA FIFA PUSKAS 2012
Shirikisho la soka la
Dunia FIFA limetangaza majina ya wachezaji kumi wanaowania tuzo ya mfungaji wa
goli bora FIFA Puskas kwa mwaka 2012. Jumla ya magoli 10 yameteuliwa na kura
zimeanza kupigwa ambapo zitapigwa hadi tarehe 29 Novemba 2012 ambapo
yatapunguzwa na kubaki matatu.
Goli bola
liatatangazwa Januari 7 2013 wakati wa ugawaji wa tuzo ya mchezaji bora wa FIFA
(FIFA Ballon d’Or 2012) jiji Zurich. Jina la Puskas limetokana na mchezaji
nguli wa Hungary Ferenc Puskas.
Magoli
yaliyochaguliwa ni:
1. Hatem
Ben Arfa: (Newcastle v Blackburn Rovers, 07 Januari 12)
2. Gaston
Mealla: (Nacional Patosi v The Strongest, 29 Januari 12)
3. Agyemang
Badu: (Ghana v Guinea 01 Februari 12)
4. Miroslav
Stoch: (Fenerbahce v Gencelerbirligi, 03 Machi 12)
6. Moussa
Sow: (Fenerbahce v Galatasaray, 17 Machi 12)
7. Eric
Hassli: (Vancouver Whitecaps v Toronto FC, 16 May 12)
8. Radamel
Falcao: (America de Cali v Atletico Madrid, 19 May 12)
9. Lionel
Messi: (Brazil v Argentina, 09 June 12)
10.
Olivia Jimnez: (Mexico v Switzerland,
22 Agosti 12)
Yatazame magoli hayo
na upige kula katika link ifuatayo:
Dumu Sports: MATOKEO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE WIKI HII
Dumu Sports: MATOKEO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE WIKI HII: Jumatano, 21 Novemba 2012 Dynamo Kiev 0-2 Paris Saint-Germain FC porto 3-0 Dinamo Zagreb Arsenal 2-0 Mo...
MATOKEO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE WIKI HII
Dynamo Kiev 0-2 Paris Saint-Germain
FC porto 3-0 Dinamo Zagreb
Arsenal 2-0 Montpellier
Schalke 04 1-0 Olympiakos
Zenit St Petersburg 2-2 Malaga
Anderlecht 1-3 AC Milan
Ajax Amsterdam 1-4 Borussia Dortmund
Manchester City 1-1 Real Madrid
Jumanne, 20 Novemba 2012
FC Nordsjaelland 2-5 Shakhtar Donetsk
Juventus 3-0 Chelsea
BATE Borisov 0-2 Lille
Vallencia 1-1 Bayern Munich
Spartak Moscow 0-3 Barcelona
Benfica 2-1 Celtic
CFR Cluj-Napoca 3-1 Braga
Galatasaray 1-0 Machester United
Dumu Sports: MAN CITY YALAMBA MCHANGA
Dumu Sports: MAN CITY YALAMBA MCHANGA: Kocha wa Man City Roberto Mancini Mabingwa wa Uingereza Manchester City jana waliaga rasmi michuano ya klabu bingwa barani ulaya kwa m...
MAN CITY YALAMBA MCHANGA
![]() |
| Kocha wa Man City Roberto Mancini |
Mabingwa
wa Uingereza Manchester City jana waliaga rasmi michuano ya klabu bingwa barani
ulaya kwa mara ya pili mfululizo. Bao la mapema la Mfaransa Karima Benzema
aliloifungia timu yake ya Real Madrid ya Hispania liliweza kuikatisha ndoto ya
Man City kuingia hatua ya 16 bora ya michuano hiyo. Katika mchezo huo timu hizo
zilitoka sare ya bao 1-1 bao lakusawazisha la Man City likifungwa Sergio Kun
Aguero kwa njia ya penati dakika 15 kabla ya mchezo kumalizika baada ya
kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari na Alvaro Alberoa ambaye alitolewa
kwa kadi nyekundu.
![]() |
| Kocha wa Arsenal Arsene Wenger |
Wakati huo huo Arsenal ilikata tiketi yake kwenye hatua ya 16 bora
baada ya kuwafunga mabingwa wa Ufaransa Montpellier kwa mabao 2-0. Mabao hayo
yalifungwa na Jack wilshere na Lukas Podolski.
ROBERTO DI MATTEO APIGWA CHINI
![]() |
| Roberto Di Matteo akifuatilia moja ya michezo alipokuwa kocha wa Chelsea |
Chelsea
imetangaza kumtema maeneja wake Mtaliano Roberto Di Matteo kwa kilichoelezwa
kutokuonesha mwenendo mzuri wa timu. Di Matteo mabaye katika uongozi wake
klabuni hapo aliingoza Chelsea maarufu kama “The Blues”michezo 42 ambapo
ilishinda 24, kupoteza 9 na kutoka sare 9. Kufutwa kazi kwa Di Matteo's kulitazamiwa
kufuatia klabu hiyo ya London kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Juventus na
kuifanya kuwa bingwa mtetezi wa kwanza kutolewa katika hatua ya makundi katika
historia ya mashindano ya klabu bingwa barani ulaya (UEFA Champions League).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotelewa na mtandao wa klabu
www.chelseafc.com,
klabu hiyo yenye uwanja wake Stanford Bridge imethibitisha kuondoka kwa Di Matteo.
Sehemu ya taarifa ilisema Chelsea imevunja mkataba na na meneja Roberto Di
Matteo. Kiwango cha mchezo na matokeo ya timu kwa siku za karibuni yamekuwa
hayaridhishi na mmiliki na bodi wameona mabadiliko ni lazima yafanyike sasa
kuiwezesha klabu kuelekea kwenye mwelekeo sahihi kwa kuwa ikielekea kwenye
kipindi muhimu zaidi cha msimu.
![]() |
| Roberto Di Matteo akisherehekea ubingwa wa UEFA Champions League na wapenzi wa Chelsea jijini London |
Klabu
hiyo ilikumbana na wakati mgumu wakati ikitafuta nafasi ya kuingia katika hatua
ya makundi za ligi ya mabingwa huku ikiendelea kupigana kubakia katika nafasi
za juu katika ligi ya nyumbani. Lengo la klabu ni kubakia katika nafasi ya
kiushandani zaidi katika mashindano yote ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
![]() |
| Roberto Di Matteo alipokuwa mchezaji wa Chelsea |
Pia
klabu hiyo imemshukuru meneja huyokwa yote mazuri aliyoifanyia klabu hiyo kubwa
hasa likiwa ni kuiwezesha kuchukua ubingwa katika ligi ya klabu bingwa barani
ulaya sanjari na kuipa ushindi wa kombe la chama cha soka cha Uingereza (FA
Cup). Klabu hiyo inasema haitaweza kumsahau Muitaliano huyo kwa mchango wake
mkubwa alioutoa ambao ni wa kihistoria katika klabu hiyo na imesema iko tayari
kumkaribisha muda wowote ule.
Wakati
huohuo klabu hiyo ikitazamiwa kumtangaza
kocha mpya wa klabu hiyo baada ya kumfukuza kazi Di Matteo, kumekuwa na kundi
linalomlaumu Di Matteo kwa matokeo mabaya katika michezo ya hivi karibuni. Katika
michezo nane ya mwisho aliwaongoza wazee wa ‘darajani’ kushinda michezo ,miwili
tu kitu kilichomplekea mmiliki wa klabu hiyo asiye mvumilivu Roman Abramovich kumfukuza
kazi.
Tuesday, November 20, 2012
Monday, November 19, 2012
MUSONYE ATANGAZA MAJINA YA MAREFA CHALLENGE
![]() |
| Katibu Mkuu wa CECAFA: Nicholas Musonye |
![]() |
| Rais CECAFA: Lodgar Tenga |
Katibu mkuu wa CECAFA
Nicholas Musonye ametangaza majina ya waamuzi watakaochezesha Tusker
Senior Challenge Cup 16
ambao 8 kati yao ni waamuzi wa wasaidizi. Wamuzi hao wanatazamiwa kupima afya
zao ijumaa tarehe 23 chini ya usimamizi wa mwamuzi anayetambuliwa na Shirikisho
la Soka Duniani FIFA Charles Masembwe.
Majina ya waamuzi walichaguliwa na nchi wanazotoka kwenye mabano ni kama ifuatavyo:
Waamuzi:
Thierry Nkurunzinza (Burundi), Maeruf Mensur
(Eritrea), Antony Ogwayo (Kenya),Hakizimana Louis (Rwanda), Ali Kalyango (Uganda),
Mohamed Hussein El Fadhil (Sudan), Denis Batte (Uganda) and Israel Mujuni
(Tanzania).
Waamuzi Wasaidizi:
Mark Ssonko (Uganda),
Mussie Kinde (Ethiopia), Peter Sabatia (Kenya), Idam Mohammed (Sudan),
Hakizimana Ambroise (Rwanda), Kinduli Ali (Zanzibar), Clemence Erasmo
(Tanzania) and Omar Abukar (Somalia).
Dumu Sports: HAYATOU KUTUA UGANDA
Dumu Sports: HAYATOU KUTUA UGANDA: Rais wa CAF: Issa Hayatou Rais wa shirikisho la soka la barani Africa (CUF) Issa Hayatou aukubali mwaliko wa shirikisho la soka la Uga...
HAYATOU KUTUA UGANDA
![]() |
| Rais wa CAF: Issa Hayatou |
Rais wa shirikisho la soka la barani Africa (CUF) Issa Hayatou aukubali
mwaliko wa shirikisho la soka la Uganda (FUFA) na CECAFA kwenda nchini Uganda.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho la soka la Uganda Hayatou anategemewa
kuwasili nchini humo tarehe 22 Novemba (Alhamisi) majira ya jioni kufuatia
mwaliko maalum aliopokea toka kwa rais wa shirikisho la soka la Uganda Lawrence
Mulindwa na rais wa CECAFA Eng. Leodgar Tenga.
![]() |
| Rais wa Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nduguCostant Omari Seleman |
![]() |
| Katibu Mkuu wa CAF Hicham El Amrani |
![]() |
| Makamu wa Rais CAF: Mohamed Raouraoua |
Katika ziara hiyo Hayatou atafuatana na maofisa mbalimbali wa CAF.
Miongoni mwa atakaombatana nao ni Katibu Mkuu wa CAF Hicham El Amran wengine
waliothibitisha ni Mohamed Raouraoua, Costant Omari na Ngangue Appolinaire.
Mara tu baada ya kuwasili na msafara wake anatazamiwa kukutana na Watendaji wa
FUFA jijini Kampala. Ijumaa tarehe 23
Novemba, atahudhuria CECAFA Congress katika hoteli ya Serena. Hayatou
anatazamiwa kuwa kusimamia ufunguzi rasmi wa CECAFA Tusker Cup katika uwanja wa Namboole siku ya jumamosi
tarehe 24, Novemba. Hayatou pia anatazamiwa kukutana na waziri wa michezo wa
Uganda Mheshimiwa Charles Bukalindi kwa mazungumzo mafupi.
Wednesday, November 14, 2012
LEON OSMAN: SIJAKATA TAMAA KUCHEZEA ENGLAND
![]() |
| Leon Osman |
Kiungo wa Everton anayemalizia
mpira wake na kuonekana kuelekea ukingoni mwa kipaji chake Leon Osman (31)
amesema hajakata tamaa na hatakata tamaa. Osman anategemea kucheza mchezo wake
wa kwanza wa kimataifa baada ya kuitwa kwa mara ya kwanza na kocha wa Uingereza
Roy Hogson.
![]() |
Leon Osman katika moja ya mechi za watani wa jadi (Derby Match) dhidi ya
Liverpool
|
England baadae leo itapambana na
Sweden katika mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na FIFA utakaofanyika jijini
Stockholm, Sweden. Leon Osman amejumuishwa kwenye kikosi cha England kilichoenda
Stockholm.
Harambee Stars Yatua Mwanza
![]() |
| Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Paulsen |
Harambee Stars ya Kenya jana
iliwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza tayari kwa mchezo wake wa leo dhidi
ya Taifa Stars. Kocha mkuu wa Wakenya hao Henri Michel amejinadi kuwa atatumia
kikosi kilekile kilichoisumbua Afrika Kusini katika mchezo wa kirafiki
uliochezwa Oktoba 16 katika uwanja wa Nyayo. Katika mchezo huo Afrika Kusini
ilipata ushindi mwembamba wa mabao 2-1.
Harambee Stars imewasili bila ya
kipa wake namba moja Arnold Origi aneyekipiga katika timu ya Ullkisa amabaye
amebanwa na ratiba ngumu ya ligi. Pia Wakenya hao watamkosa mshambuliaji wao
hatari Victor Wanyama ambaye anakabiliwa na majeruhi. Michel amemuita Jactone
Odhiambo wa Ulinzi kuziba pengo la Origin a Anthony Akumu wa Gor Mahia kuziba
pengo la Wanyama.
Naye kocha wa Taifa Stars Kim
Paulsen amefanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi chake kwa kuwaacha Said
Bahanuzi (Yanga) na Haruna Moshi “Boban” (Simba). Paulsen ameongeza kiungo
hatari Amri Kiemba (Simba) pamoja na damu changa kama Frank Domayo (Yanga),
Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba). Pia katika kikosi hicho
hakuwaacha wachezaji wenye asili ya visiwani ambao wataruhusiwa kujiunga na
Zanzibar Heroes mara tu baada ya mchezo wa Leo. Wachezaji hao ni Aggrey Morris,
Said Nassor “Cholo”, na Issa Rashid.
THE CRANES KUIVAA HARAMBEE STARS
![]() |
| Timu ya taifa ya Kenya "Harambee Stars" |
Timu ya soka ya Uganda The Cranes
itashuka dimbani kuikaribisha timu ya taifa ya Kenya almaarufu Harambee Stars.
Timu hizi zitachuana katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya CECAFA Challenge
Cup mchezo utakaochezwa tarehe 24 Novemba mwaka huu jijini Kampala.
![]() |
| Timu ya taifa ya Uganda "The Cranes" |
The cranes bado wana uchungu wa
kubaniwa na Harambee Stars nafasi ya kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika. Katika
mchezo huo Wakenya hao waliilazimisha The Cranes sare isiyo na magoli (suluhu),
mchezo huo ulifanyika huko Namboole. The Cranes pia katika mchezo wake wa
mwisho ilifungwa kwa penati 8-9 na Zambia hapohapo Namboole mwezi Januari mwaka
huu.
Kabla ya mechi hiyo ya ufunguzi
timu za Ethiopia na Sudani Kusini zitapambana katika mchezo unaotazamiwa kuanza
majiara ya saa tisa (9) alasiri kwa saa za Afrika Mashariki. Kwa sasa Uganda
ipo katika nafasi ya 88 na Kenya ipo katika nafasi ya 130 ya ubora wa viwango
vya soka duniani.
Tuesday, November 13, 2012
STARS KUKIPIGA NA HARAMBEE STARS
![]() |
| Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Picha kwa hisani ya tff.or,tz |
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars inatazamia kushuka katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza kesho jumatano tarehe 14 itakapo wakaribisha Harambee Stars ya Kenya. Taifa Stars na Harambee Stars zitakwaana katika mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Kwa mujibu wa mtandao wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Tanzania tff.or.tz, mchezo huo unatazamiwa kuanza majira ya saa 10 jioni. Mchezo huu ni muhimu kwa timu zote mbili, ambapo kwa upande wa Kenya itakuwa ikijipima nguvu kujiandaa na mchezo wa hatua ya makundi wa kuwania nafasi ya kushiriki kombe la dunia na pia kama ilivyo kwa Taifa Stars pia mchezo huo ni maandalizi ya michuano ya kombe la CECAFA Challenge.
Taifa Stars kwa sasa ipo katika nafasi ya 134 katika viwango vya soka duniani, itaingia dimbani kuchuana na Kenya iliyo katika nafasi ya 130. Mbali na maandalizi ya CECAFA Challenge Cup, mchezo huo ni muhimu kwa Stars inayopigana kurejea katika kiwango chake juu, ambapo katika historia ni nafasi ya 65 ambayo ilifikiwa mnamo mwaka 1965.
Friday, November 9, 2012
Wenger Alegeza Msimamamo Wake
![]() |
| Jack Wilshere |
Meneja wa washika
bunduki wa London Mfaransa Arsene Wenger amelegeza msimamo wake na kumrushusu mchezejai
wake Jack Wilshere (20) kuchezea timu ya taifa ya Uingereza itakapopambana na
Sweden wiki ijayo. Awali
Wenger alimtaka kocha wa Uingereza Roy Hogson kumpumzisha mchezaji huyo kwa
kuwa alikuwa majeruhi kwa muda mrefu. Mameneja hao walifikia muafaka wa kumruhusu
Wilshere mara baada ya mchezo kati ya Arsenal na Manchester United ambapo
Wilshere alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Akiongea na skysports.com Wenger alisema "Ninaona ni mapema mno kwa Jack
lakini nimeongea na Roy Hodgson kwa simu na tumeelewana na kufikia muafaka
mzuri”
"Kizuri zaidi ni kuwa hatacheza mwishoni
mwa wiki hii kwa kuwa na adhabu ya kadi nyekundu hivyo atapumzika na kujiunga
na kikosi kama Roy anavyotaka”
Subscribe to:
Comments (Atom)











































